“Hivi tuwaze kidogo hapa Wana Simba wenzangu yaani unajua fika unakwenda kucheza derby ya kariakoo ambayo inakwenda kuamua Bingwa wa nchi ligi kuu TANZANIA BARA unakwenda kucheza na mtani wako wa jadi Yanga ambaye mechi iliyopita alikufunga Bao MOJA KWA bila YOTE haya unayajua kwenye mechi hii muhimu yenye hisia na msisimko mkubwa ila Bado unapeleka kikosi cha wachezaji ambao wanadai mishahara na posho zao hujawalipa pesa ambayo Muwekezaji Tayari ameshaitoa kwenu uongozi zaidi ya wiki moja nyuma.
Tajiri ametoa pesa ili wachezaji walipwe mishahara na posho zao Kisha hujawapa hizo pesa wewe umebakia nazo Kisha unataka wacheze washinde mechi ya derby how?
Kisha unatarajia wachezaji Hawa waende uwanjani wakajitoe na kujituma kupata matokeo wakiwa na njaa dhidi ya timu ya ambayo bosi wao amewapa Bilioni moja wamelala nayo ili wakachukue Ubingwa? Utaweza kweli kushindana na timu ya aina hiyo? “
By Doctormohamedihamisi’s via Instagram