Tetesi za Dabi ya Yanga na Simba Kupangiwa Tarehe Nyingine

Tetesi za Dabi ya Yanga na Simba Kupangiwa Tarehe Nyingine


Taarifa za awali kutoka katika vyanzo mbalimbali vya habari za michezo nchini Tanzania zinaeleza kwamba TFF na bodi ya ligi wanafikiria kupeleka mbele mechi ya dabi ya kariakoo ambayo imepangwa kupigwa tarehe 15 Juni, katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.


Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya mamlaka hizo zinaeleza kwamba mpaka sasa Yanga Sc wameshikilia msimamo wao wa kugomea mechi hiyo, TFF na bodi ya ligi hawana namna yoyote ya kufanya zaidi ya kubadilisha tarehe ya mchezo huo.


Yanga Sc walitoa matakwa manne ambayo yanapaswa kufanyiwa kazi na mamlaka hizo ili wao wakubaliane na ratiba ya kucheza mechi hiyo, TFF na bodi ya ligi wanataka kusogeza mbele mechi hiyo ili wapate muda wa kuendelea kufanya majadiliano na klabu ya Yanga Sc.


TFF na bodi ya ligi hawako tayari kufuata matakwa ya klabu ya Yanga Sc na sasa wanatafuta namna nzuri ya kumaliza sakata hili ili angalau Yanga Sc wakubaliane na ratiba ya kucheza mechi hii kubwa kwenye historia ya soka la Tanzania bara.


Bodi ya ligi na TFF kwa sasa wameshikwa pabaya na viongozi wa klabu ya Yanga Sc na ndio maana imekuwa kazi ngumu kwa wao kukubaliana na maamuzi ya klabu ya Simba Sc ambao mpaka sasa wanashinikiza kwamba mechi hiyo ipigwe kama ilivyokua imepangwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad