Nimepitia kwa utulivu matakwa ya Nyuma Mwiko waliyowasilisha Bodi ya Ligi nimeona kuna usela mwingi baadala ya hoja za msingi
Unataka Katibu Mkuu wa TFF ajiuzulu?!! Kwa kushindwa kusimamia waamuzi
Pengine hamjui kazi za Katibu Mkuu, Jukumu lake ni kuandaa Kozi za Waamuzi, kuboresha maslahi yao na kuadhibu Wanaokosea yote hayo yanafanyika kwa asilimia mia moja.
Mafanikio ya leo kwenye mpira wa miguu ni kutokana na mchango wa Mtendaji Mkuu akisimamiwa vema na Rais Wallace Karia na Kamati yake ya Utendaji
Timu zetu za Taifa za madaraja yote zinapishana kwenye michuano ya Afrika hii ni kazi ya Katibu Mkuu
Siko hapa kuelezea mafanikio yake lakini itoshe kusema tuu mpira wa miguu hauko tayari kupoteza Lulu kwa maslahi ya Yenu
Wanataka pia Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Almas Kasongo nae ajiuzulu
Kwa kosa gani?!! Ubaya wa Kasongo umeanza lini?
Wakati mnachukua Ubingwa mara tatu hamkuona ubayaa wa Kasongo
Kasongo huyu chini ya Utawala wake Ligi yetu imeshika nafasi nne kwa ubora wa Afrika
Vipo vilabu vinajiendesha kwa fedha kutoka kwa Wadhamini waliotafutwa na Bodi ya Ligi ya Kasongo
Tuaambie tuu hatujajiandaa kumpoteza Kasongo hivi sasa mazuri yake ni mengi kuliko ubaya mnaompakazia
Ninachokiona mimi haya ni mapambano ya kutaka kuweka watu wenu kwenye nyadhifa hizo
Na sio watende haki bali wasimamie maslahi yenu, Hatuwezi kuruhusu hilo litokee
Mikwara ya kuwa hutashiriki ligi msimu ujao mpaka matakwa yako yafanyiwe kazi, Huo ni mkwara wa Bata
Mpira wa Nchi hii unaweza kwenda bila wewe na watu wakafurahi
Amepotea Pan Africa, Red Star na Cosmpolitan wewe nani
By the way timu yenu ni Sports Club mkiona mpira umewashinda nendeni mkacheze Boxing au Basketball