Bodi ya Ligi: Dabi ya Kariakoo Ipo Pale Pale, Maandalizi Yanaendelea

Bodi ya Ligi: Dabi ya Kariakoo Ipo Pale Pale, Maandalizi Yanaendelea


Afisa Habari wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, Karim Boimanda, amesema kuwa maandalizi ya mchezo wa Dabi ya Kariakoo yanaendelea kama kawaida, huku akibainisha kuwa mchezo huo una umuhimu mkubwa kwa taswira ya Ligi Kuu ya Tanzania.

"Tunaendelea na maandalizi na ni matumaini yetu kuwa wadau wengine, zikiwemo hizo timu mbili za Yanga na Simba, nao wanaendelea na maandalizi kuelekea huo mchezo. Ni mchezo mkubwa, mchezo ambao ni kioo cha ligi yetu,” amesema Boimanda.

Aidha, ameeleza kuwa baadhi ya taarifa muhimu na nyeti kuhusu mchezo huo zitatolewa muda wowote kuanzia sasa, akiwataka wadau na mashabiki wa soka kufuatilia kwa karibu taarifa rasmi kutoka Bodi ya Ligi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad