Klabu ya Young Africans SC kupitia taarifa yake imeeleza wazi kuwa haijawahi kupokea malipo yoyote ya zawadi ya ubingwa wa Kombe la Shirikisho kwa misimu mitatu mfululizo kuanzia 2021/2022 hadi 2023/2024 ambapon wamedai kuwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kushikilia fedha hizo bila sababu halali, jambo ambalo ni kinyume cha utaratibu na hakuna uthibitisho wowte ukionesha kuwa wamewahi kulipwa.
Aidha Klabu hiyo imesema haitambui deni lolote kwa TFF na inasisitiza kuwa malipo haya yanapaswa kufanyika kwa wakati ili kuheshimu mshindi na utawala bora wa mashindano.
Uongozi wa Young Africans SC umeeleza kuwa unahitaji TFF iwalipe deni la msimu wa 2023/2024 haraka iwezekanavyo ili klabu iweze kushiriki fainali itakayofanyika Juni 28, 2025, bila vikwazo vya kifedha.