Simba Watoa Msimamo, Tutashiriki Dabi Tarehe 15, Zaidi ya Hapo Hatuchezi

Simba Watoa Msimamo, Tutashiriki Dabi Tarehe 15, Zaidi ya Hapo Hatuchezi

Klabu ya Simba imetoa taarifa rasmi ikieleza kuwa itashiriki mchezo wa Ligi Kuu namba 184 dhidi ya Yanga Sc kama ulivyopangwa kufanyika siku ya Jumapili, tarehe 15 Juni 2025.

Klabu hiyo imesisitiza kuwa haitakubali mabadiliko yoyote ya ratiba ya mchezo huo kwani ni kinyume na taratibu za uendeshaji wa mpira wa miguu nchini.

Kupitia taarifa hiyo uongozi wa Simba umehimiza Wanachama na mashabiki wake kujitokeza kwa wingi kujaza Uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya mchezo ili kuiunga mkono timu yao katika mchezo huo.

Simba Watoa Msimamo, Tutashiriki Dabi Tarehe 15, Zaidi ya Hapo Hatuchezi

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad