Kimenuka Simba, Baadhi Wataka Mangungu Ajiuzulu, Mwenyewe Afunguka Haya



Mwanachama wa klabu ya Simba SC Dinnah amesema kuwa kitendo cha timu ya Simba SC kukaa misimu minne bila kikombe kinatosha kwa Mwenyekiti wao Murtaza Mangungu kungatuka madarakani. Mwanachama huyo aliyekuwa na wanachama wengine katika uwanja wa Gwambina Temeke jijini Dar es. Wamesema hawana imani na Mwenyekiti huyo kutokana na hali ya mambo kwenye klabu hiyo.


Aidha Murtaza Mangungu amevunja ukimya wake baada ya tuhuma kuhusu wachezaji kudai pesa zao.

Akizungumza kwa hisia, Mangungu amesema hawezi kuwalaumu watu hao kwa sababu kila mtu ana mtazamo wake, lakini amesisitiza kuwa watu hao wanapaswa kwanza kueleza makosa aliyoyafanya kabla ya kumtaka aondoke.

Mangungu ameonesha dhahiri kuwa kuna baadhi ya watu ambao hutokea tu pale timu inapofanya vibaya, huku wakikaa kimya wakati mambo yanapokuwa mazuri.

Amesema baadhi ya wanaomkosoa wanaendekeza siasa za uchaguzi na hawaitakii klabu mema kwa dhati, bali wanatumia changamoto za muda mfupi kama kigezo cha kuibua malalamiko ya uongozi.

Katika kauli yake, Mangungu amesisitiza kuwa Simba ni taasisi yenye mfumo wa kiuongozi, siyo mtu mmoja, hivyo maamuzi yote muhimu hufanywa kwa pamoja na si kwa misingi ya mtu binafsi.

Ametolea mfano kuwa hata kama jina lake linasikika sana kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, hiyo haimaanishi kwamba yeye peke yake ndiye anayeendesha klabu, bali ni sehemu ya timu kubwa ya viongozi.

Pia amesema kuna kundi la watu linaloonekana kufurahia matatizo ya klabu kuliko mafanikio yake. Amewataka wanachama na mashabiki kuwa na mtazamo mpana zaidi, kuwa wavumilivu, na kuielewa Simba kama taasisi yenye mipango na malengo ya muda mrefu ambayo yanahitaji mshikamano na siyo lawama za mara kwa mara.




Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad