Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi amemtangaza rasmi Bw. Rashid Mijuza kuwa Kaimu Meneja wa Uwanja wa Benjamin Mkapa baada ya kumhamisha na kumpeleka Makao Makuu ya Wizara hiyo aliyekuwa Meneja wa Uwanja huo Bw. Malinde Mahona ambaye atakuwa msimamizi wa viwanja vyote nchini.
Waziri Kabudi amesema hayo Mei 10, 2025 alipofanya ziara maalumu ya ukaguzi wa Kiwanja hicho na viwanja vya Mazoezi ya CHAN 2024 akiongozana na Katibu Mkuu Wizara hiyo na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa jijini Dar es salaam.