Gamondi awa mbogo kisa Mzize na Guede

Gamondi awa mbogo kisa Mzize na Guede


Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi amegeuka mbogo kwa Mwandishi wa habari aliyeuliza kwanini amemuazisha kijana mdogo Mzize na kumuacha Joseph Guede mkomavu na mwenye uzoefu na michuano mikubwa, wakati wa mkutanao wa waandishi wa habari baada ya mchezo.


Gamondi amefunguka hayo wakati akihojiwa na wanahabari baada ya mchezo wa Robo Fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga na Mamelodi Sundowns, mchezo ambao ulimalizika kwa sare ya bila bila kufungana katika Dimba la Mkapa.


"Mzize ni 'future' ya Tanzania sio Yanga tu, sasa atapataje uzoefu kama hapati nafasi ya kucheza, mbona kacheza vizuri sana, katengeneza nafasi nyingi, kukosa ni kawaida kwa washambuliaji, au hujaona alichokifanya?


"Wewe ni mwandishi wa habari nadhana una uelewa wa mambo kuliko shabiki, sasa unaulizaje swali kama shabiki, haya nami nikuulize yule Peter Shelulile wa Mamelod Sundowns katengeneza nafasi ngapi?" Amesema Gamondi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.