Kocha Mamelodi aukubali mziki wa Yanga

Kocha Mamelodi aukubali mziki wa Yanga


Kocha Mkuu wa Mamelodi Sundowns FC, Rulani Mokwena amesema amekutana na Yanga ngumu ndani ya dakika 90' kama alivyotarajia katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, ingawa imani yake ni kuwa watafuzu hatua ya Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL).


Amesema hayo katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kutamatika mchezo wa hatua ya Robo Fainali ya CAFCL dhidi ya wenyeji Yanga kwa suluhu ya bila kufungana.


"Ninaamini tunaenda kufuzu kwakuwa malengo yetu katika mchezo huu ni kurudi nyumbani tukiwa na hati safi," amesema Mokwena


Mchezo wa mkondo wapili wa hatua ya Robo Fainali utachezwa Aprili 05, 2024 katika Uwanja wa Loftus Versfeld ndani ya Jiji la Pretoria, Afrika Kusini.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.