John Bocco Ndio Basi Tena Msimbazi, Simba Kuwatema Watano
SAFARI ya misimu saba ndani ya Simba kwa mshambuliaji John Bocco inakaribia ukingoni baada ya uongozi wa klabu hiyo kumtoa kwenye mipango yao ya msimu ujao. Simba sasa inajiandaa kuachana na wachezaji wake wasiopungua WATANO kwenye dilisha dogo hili la usajili huku wengine wakisubiriwa mwisho wa msimu ufike wamalize mikataba yao na kuondoka huru.
Uongozi wa Simba tayari umemalizana na Bocco kwa kumpa uhuru wa kuchagua kuondoka Msimbazi kwenye dilisha dogo linalotarajiwa kufunguliwa Disemba 16, mwaka huu na kama ikishindikana basi atasubiri hadi mwisho wa msimu mkataba wake umalizike aondoke.
Tayari staa huyo aliyeingia Msimbazi mwaka 2017 akitokea Azam, ametolewa kwenye mipango ya kocha mpya Abdelhak Benchikha. Akiwa Simba, Bocco alitwaa mataji manne ya ligi mfululizo kuanzia msimu wake wa kwanza unyamani 2017/2018 hadi 2021/2022 pia kwa nyakati tofauti amekuwa mshambuliaji kinara akiibuka mfungaji bora wa ligi msimu wa 2020/2021 (mabao 16). The Legend John Bocco ‘Adebayor’