Hesabu za Haji Manara Hizi Hapa Yanga Kutoboa Katika Kundi lake Ligi ya Mabingwa


Hesabu za Haji Manara Hizi Hapa Yanga Kutoboa Katika Kundi lake Ligi ya Mabingwa

Hesabu za Haji Manara Hizi Hapa Yanga Kutoboa Katika Kundi lake Ligi ya Mabingwa


"Tunahitaji sana ushindi kesho pale Kumasi tutakapokuwa tukienda kucheza na FC Medeama ya kule nchini Ghana, lakini mimi binafsi hainipi Presha ikitokea vinginevyo.

Tutashukuru na kufurahi sana tukipata alama tatu away, lakini tutasema asante Mungu ikitokea hata sare, ingawa najua tunao Wachezaji wakubwa wanaoweza kushinda hiyo kesho.

Labda kwa nini nasema tukipata hata droo is not bad, ni namna mwenendo wa Group letu jinsi lilivyo, mathalan ikitokea hivyo kisha tukaja kupata matokeo home kwenye Mechi ya Marudiano, tutakuwa na alama tano huku wenzetu wakibakia na alama zao nne.

Na Wale Waarabu wakagawana Points Tatu Tatu maana yake tutakapokuwa tukiwakabili Waalgeria kwa mkapa, ni Mechi ya Do Or Die tukishinda tu itakuwa tunaelekea kutoboa na hasa kama Ahly atakuwa amepata Points nyingi na Waarabu wenzao pamoja na Mechi yao na Medeama.

Ni hesabu tu na football ipo hivyo, nzuri zaidi ni alama sita dhidi yao na InshaAllah INAWEZEKANA 🙏🙏"

Ameandika Aliyekuwa msemaji wa Yanga, Haji Manara kwenye ukurasa wake wa Instagram kuelekea mechi yao dhidi ya Medeama hapo kesho


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.