Viwango Vimeshuka Au Mfumo Mpya wa Gamondi Umewatema Hawa?


Viwango Vimeshuka Au Mfumo Mpya wa Gamondi Umewatema Hawa?


Back to 2022/23

Kikosi kilichoshinda ubingwa wa Ligi kuu msimu wa 2022/23 Ubavu wa kulia alikuwa mali ya Kibwana Shomari na mara kadhaa alikula mbavu ya kushoto , Farid Mussa alipewa pia ubavu wa kushoto au winga kulingana na namna Nabi alivyoamka ,kwa Sure Boy yeye pale kati alianza kujenga utawala wake na Doctor Khalid Aucho.

Kikosi kilichotwaa ubingwa wa FA hivyo hivyo na hata kikosi kilichoifikisha Yanga fainali ya CAFCC wafia timu walikuwa hawa .

Nimewataja hawa kwa sababu walikuwa wanapata sana nafasi ili iwe rahisi kujadili na kuelewana.

2023|24 ,Benchi linaongozwa na Gamondi ambaye amekuja na usajili kwenye baadhi ya nafasi ,vijana hawa pichani kazi yao imekuwa kufanya mazoezi na timu na kusafiri ili kukamilisha idadi ya wachezaji wanaosafiri na timu .

Baadhi yao huwaoni hata wakikaa benchi ,baadhi wanakaa benchi na kupewa dakika chache inapobidi .

Swali la kujiuliza hapa, viwango vimeshuka ,wameridhika au mfumo umewakataa kwa maana maingizo mapya ni daraja la juu kuwazidi ___?

Hapa hakuna mlango wa lawama kwa maana anapokuja bora zaidi yako unatakiwa kujiboresha ili kuleta ushindani ,tulitazame na kulichambua kwa upande huo pia ili tuweze kupata muafaka nini kimewaweka kwenye mbao ndefu ?

Source: Shaffih Dauda

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad