Liverpool Waichapa Everton Dabi ya Merseyside Ligi Kuu ya England

 

Liverpool Waichapa Everton Dabi ya Merseyside Ligi Kuu ya England

WENYEJI, Liverpool FC wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Everton katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Oktoba 21 Uwanja wa Anfield Jijini Liverpool.


Shujaa wa Liverpool alikuwa ni mshambuliaji wa Kimataifa wa Misri, Mohamed Salah aliyefunga mabao yote hayo, la kwanza kwa penalti dakika ya 75 na la pili dakika ya 90 akimalizia pasi ya nyota wa Uruguay, Darwin Nunez.


Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 20 na kusogea nafasi ya tatu, ikizidiwa pointi moja mabingwa watetezi, Manchester City na Arsenal waliopo nafasi ya pili wakati Everton inabaki na pointi zake saba nafasi ya 16 ligi ya timu 18 baada ya wote kucheza mechi tisa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.