Geita Gold, Dodoma Jiji Hakuna Mbabe

Geita Gold, Dodoma Jiji Hakuna Mbabe

 

Geita Gold wamekubali kugawana pointi mojamoja na wapinzani wao Dodoma Jiji kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Nyankumbu baada ya dakika 90 ubao umesoma Geita Gold 2-2 Dodoma Jiji.


Mchezo huo ulikuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote kuonyesha uwezo kusaka pointi tatu ndani ya dakika 90 za mchezo.


Ni Geita Gold walianza kupata bao la kuongoza dakika ya 10 kupitia kwa Tariq Seif huku Dodom Jiji mabao yote yakifungwa na nyota Hassan Mwaterema dakika ya 62 na 64.


Bao la kuipa pointi moja Geita Gold limepachikwa dakika ya 86 mtupiaji ni Hassan Mahamoud.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.