Timu ya Singida Big Stars imeibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya wenyeji, Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Jana Jumamosi Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
Mabao ya Singida Big Stars yamefungwa na viungo Mkenya, Duke Ooga Abuya dakika ya 45 na ushei na Mtogo, Marouf Tchakei mawili dakika ya 68 na 81, wakati ya Namungo FC yamefungwa na Derick Mkombozi dakika ya 64 kwa penalti na Emmanuel Charles dakika ya 90 na ushei.
Kwa ushindi huo, Singida Big Stars inafikisha pointi nane na kusogea nafasi ya sita, wakati Namungo FC inabaki na pointi zake tatu nafasi ya 14 kwenye Ligi ya 16 baada ya wote kucheza mechi sita.