Ratiba ya Ligi Kuu hiyoo!

 

Ratiba ya Ligi Kuu hiyoo!

Wakati wadau na mashabiki wa soka nchini wakisubiri kuanza kwa Ligi Kuu msimu wa 2023/24 bodi ya ligi hiyo nchini (TPLB) imesema ratiba ya mashindano hayo wataiachia siku mbili zijazo.


Ligi Kuu inatarajia kuanza Agosti 15, huku ikishuhudiwa baadhi ya timu zilizokuwapo msimu uliopita zikikosekana, huku zikitokea mpya tatu kwa michuano hiyo.


Timu za Mbeya City, Ruvu Shooting na Polisi Tanzania zilizokuwapo msimu huo, hazitakuwapo baada ya kushuka daraja, huku Tabora United, Mashujaa na JKT Tanzania zikichomoza msimu ujao.


Hadi sasa timu, mashabiki na wadau wa soka nchini wanasubiria kujua rariba inatoka lini ili kujua nani anaanza na nani na wapi ili kuanza mipango na mikakati rasmi.


Ofisa Habari wa bodi ya Ligi Kuu chini (TPLB), Karim Boimanda amesema hadi sasa ratiba imeshakamilika na muda wowote kuanzia kesho Jumapili au Jumatatu wataiachia rasmi.


Amesema wamechelewa kuitoa kutokana na shirikisho la soka Afrika (CAF) kuchelewesha kalenda yao huku akibainisha wameboresha na huenda changamoto za kusimamisha au kusogeza mechi zisijitokeze kama ilivyokuwa msimu uliopita.


"Kuanzia kesho hadi Jumatatu ratiba itatoka rasmi kujua nani anaanza na nani na wapi, tumechelewa kutokana na kutopata mapema kalenda ya CAF, lakini tumezigatia ratiba ya michuano ya kimataifa hivyo zile changamoto za msimu uliopita hatutarajii kujitokeza"


"Ni ngumu ligi kukosa mapungufu kwa sababu kuna ratiba zinaweza kujitokeza za dharula, lakini sisi tumejitahidi kurekebisha kadri ya uwezo wetu ili kuondokana na hilo" amesema Boimanda.


Ofisa habari wa Tanzania Prisons, Jackson Mwafulango amesema wao wapo tayari kukutana na yeyote na popote kwani kikosi chao kipo fiti kwa ajili ya msimu ujao.


"Sisi hatuna presha wala wasiwasi tumejipanga kuanza na yeyote na popote, iwe nyumbani au ugenini, tupo kambini mazoezi yakiendelea tangu Julai 3," ametamba Mwafulango.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.