Ahmed Ally: Mwanasimba Ficha Tiketi yako, Usimuamini Hata Ndugu yako

Ahmed Ally: Mwanasimba Ficha Tiketi yako, Usimuamini Hata Ndugu yako


 Meneja wa Habari na Mawasilino Simba SC Ahmed Ally amesema Mashabiki na Wanachama wa Klabu hiyo wenye tiketi za Simba Day wajitahidi kuzilinda.


Kesho Jumapili (Agosti 6) ni kilele cha Simba Day ambapo Simba SC watafanya tamasha lao kwa kutambulisha wachezaji wapya na wale waliokuwa katika kikosi cha msimu wa 2022/23.


Miongoni mwa wachezaji wapya ndani ya Simba ni Fabrice Ngoma ambaye alikuwa anatajwa kuwa kwenye hesabu za Young Africans.


Litakuwa tamasha la tatu kwa ukubwa baada ya Young Africans kukamilisha Wiki ya Mwananchi ambalo ni la Young Africans kisha Singida Fountain Gate wao ni Singida Big Day.


Young Africans walifanyia Uwanja wa Benjamin Mkapa sawa na Simba SC huku Singida Fountain Gate walifanyia tamasha lao mkoani Singida, Uwanja wa Liti.


Mgeni Rasmi katika Tamasha Simba Day anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ikiwa ni taarifa rasmi iliyotolewa na Simba SC jana Ijumaa (Agosti 4).


Ahmed amesema: “Mwenye tiketi ya Simba Day ajitahidi kuificha yaani usimuamini hata ndugu yako wa karibu anaweza kupita nayo ukamkuta uwanjani,”


Taarifa kutoka Simba SC zimeeleza kuwa tiketi zote zimeisha kwenye kila eneo ikiwa ni kuanzia Platinum, mzunguko mpaka VIP.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.