Mamelodi Sundowns Hawana Nyumbani Wala Ugenini...Dozi Inatolewa Popote

Mamelody

Mamelodi Sundowns ni miongoni mwa timu bora Afrika ambayo inacheza kwa kiwango cha juu sana. Kwa sasa haina nyumbani wala ugenin, inashinda popote.


Hiyo imedhihirika kwenye mechi yao ya ugenini dhidi ya Wydad Casablanca ambapo mchezaji wao alikuwa ‘umeme’ mapema kabisa lakini walicheza kama wametimia.


Dakika za mwishoni mchezaji mwingine tena wa Mamelodi akaoneshwa kadi nyekundu mechi ikaisha mamelodi ikiwa na wachezaji tisa uwanjani lakini hawakuruhusu goli!


Kwa hiyo mechi ya marudiano wakiwa nyumbani watakuwa na nafasi nzuri ya kupata ushindi na kwenda Fainali kucheza dhidi ya Al Ahly ambayo inapewa nafasi kubwa ya kwenda Fainali baada ya kuifunga Esperance 3-0 kwenye mechi ya kwanza.


Lakini mpira una maajabu yake, huwezi kuongea na kumaliza maneno yote, Al Ahly pamoja na kushinda 3-0 ugenini dhidi ya Esperance bado tunahitaji kusubiri kwa sababu Esperance sio timu ya kubeza.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.