Wallace Karia Amshtaki HAJI Manara Kwa Kumchafua, Aitwa Polisi

Wallace Karia Amshtaki Haji Manara Kwa Kumchafua, Aitwa Polisi



RAIS wa Shirikisho la Soka Nchini Tanzania (TFF), Wallace Karia, amemshitaki Mwanachama wa Yanga SC. Haji Sunday Manara kwa tuhuma za kuchapisha maandiko mbalimbali kwenye mitandao yake ya kijamii ya kumtaka Rais huyo ajiuzulu kwa tuhuma za TFF kudaiwa na Yanga.


Haji Manara alifikishwa Polisi leo Juni 13, 2025 mpaka majira ya saa 4 asubuhi kwa mahojiano zaidi lakini kwa sasa tayari amechiwa baada ya kupata dhamana.


Akithibitisha tuhuma hizo Kamanda wa Polisi Kanda maalumu Dar es Salaam SACP. Jumanne Muliro amesema: “Ni kweli Haji Manara amehojiwa baada ya kupata malalamiko kutoka kwa Rais wa TFF, akilalamika kuhusiana na Manara, Jukumu letu sisi lilikuwa ni kumuita na kumuhoji juu ya malalamiko dhidi yake.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad