Yanga wanamtaka Fei Toto kuziba pengo la Aziz ki kwenye kikosi Chao. Yanga ambayo ilimuuza kwa nguvu Fei Toto kwenda Azam Fc, nayo imefanikiwa japo kuumaliza mgogoro kati yao na kijana wao huyo, Kisha hapo hapo ikampa ofa nono kiungo huyo ili arejee jangwani.
Yanga imemwambia Fei Toto atakapo kubali kurejea jangwani, hatarejea tena kinyonge, hakuna tena masuara ya ugari na sukari, kwani itamkabidhi fedha za kufuru ikimuwekea ofa ya sh 800 million, pia itampa mshahara anaoutaka wa million 40 kwa mwezi, ambao Azam pia wanataka kumpa atakapo kubali kuongeza mkataba mpya.
Azam kwa sasa inamlipa mshahara wa sh million 23.5 kwa mwezi ambapo ukiondoa Kodi zote kwenye akaunti yake inaingia million 15 kama mshahara, mkataba huo ukiwa na thamani ya million 390 kama ada ya usajili.
Mbali na ofa hiyo, yanga pia imemtaka Fei achague kujengewa Nyumba anapopataka lakini pia atapewa gari la kifahari kwenye dili hilo lakini pia wakimwambia kumalizana na Azam awaachie wao wanajua watakapo malizana na mabosi hao.