."Nakiri msimu huu sijafanya mambo makubwa sana, hili limetokana na uchovu wa msimu uliopita na nilipambana sana kuweka sawa malengo ya klabu."
"Sio Yanga tu, pia hata timu ya Taifa langu Burkina Faso, nako sikuwa na muendelezo mzuri, lakini sasa akili yangu imetulia na inarudi uwanjani."
“Bahati mbaya nilipata maumivu ya mgongo, lakini nitakapokuwa sawa ninataka kuanzia hapa kwenye klabu yangu mpaka timu ya Taifa kufanya mambo makubwa."
"Najua ambacho watu wanasema ninapokuwa sijafanya mambo makubwa, na ni kwa sababu wanatarajia vingi kutoka kwangu, hivyo nitahakikisha narudisha kiwango wanachotaka mashabiki."
Aziz Ki amesema ishu hiyo ya kubadilishwa makocha nayo imechangia kutokuwa na mwendelezo mzuri.
"Sababu nyingine iliyonitatiza ni mabadiliko ya makocha Yanga na yalihitaji ujasiri kwetu kama wachezaji kubadilika kwa haraka, pia majeraha madogo madogo na vyote hivi viliondoa utulivu wa kufanya muendelezo wa kiwango changu."