Pengine hizi zitabaki kuwa ni fikra zangu tu! Lakini yote ilikuwa ni usajiri tu! Ukiitizama Yanga SC ambayo iliwachukuwa takribani miaka 5 hadi 4 kurudi katika ubora wake na kushinda mataji mbele ya Simba na Azam, ilikuwa ni usajiri tu!
Kipindi kile Simba anashinda mataji ya Ligi Kuu Mara 4 mfululizo mbele ya Yanga SC, ilikuwa ni usajili tu!
Kule Yanga kulikuwa na usajili usiyoendana na ukubwa wa klabu, pia ulikuwa haulingani ubora na mahasimu wao ambao ni Simba wakionekana ni bora kila idara na kushinda mataji mara 4 kwa sababu Simba walikuwa na usajiri bora kuliko watani zao Yanga, ilikuwa ni usajiri tu!
Simba kulikuwa na akina kachi kahata, Louis Miquissone, Chama, Meddie Kagere, John Bocco, Hassan Dilunga, Emmanuel Okwi, Deo Kanda, Gyan na wengine. Wote wakiwa kwenye ubora na wakiitumikia Simba kwa faida kubwa, wengine wakauzwa, wengine wakabaki, na wengine wakaachwa, yote ilikuwa ni usajiri tu!
Kule Yanga kulikuwa na akina Sadney Urikhob, Lamine Moro, Juma Balinya, Yikpe, Dadid Molinga, Makambo, Michael Sarpong, Jimmy Kindoki na wengine wengi. Wachezaji wote hao waliitumikia Yanga kwa hasara kubwa ndani ya miaka minne wakipishana kwenye madawati ya viongozi wa Yanga kufanya usajiri, lakini yote ilikuwa ni usajiri tu!
Leo Yanga wakawaza na kuwazua wakagundua nini kinachowafelisha hadi kushindwa kubeba ubingwa miaka 4, wamegundua tatizo lao kubwa ni usajiri tu!
Yanga wakaingia sokoni, wakamleta Djugui Diarra kwa pesa nyingi, yanga wakasafiri hadi Congo wakawafuata akina Mayele, Bangala, Moloko, Djuma Shaban, na wengine wengi wakiwemo mastaa wa ndani, wakavunja uteja wa miaka 4 kwa kubeba ubingwa msimu wa 2021-2022, kwa sababu yote ilikuwa ni usajiri tu!
Yanga hawakuishia hapo, kwa sababu walishagundua matatizo yao ndani ya miaka minne ni usajiri, wakasafiri hadi nchini Burkna Faso wakamchukua Ki Aziz kwa pesa nyingi, hawakujali kwa sababu walishaamini kwenye usajiri tu.
Hawakuishia hapo kwenye dirisha dogo wakamleta musonda nakuifanya timu yao kuwa na utulivu wa kikosi kila idara, kwa sababu ni usajiri tu!
Mimi binafsi ukinifuata kuhusu tatizo la Simba, nitakwambia ni “usajili tu”, tazama kwenye benchi la Simba, kuna Kyombo, Gadiel, Nyoni, Kapama, Banda ambaye ndiyo alikuwa mbadala wa Lous Miquissone, ameshindwa kabisa kuingia kikosi cha kwanza.
Sikumbuki mara ya mwisho lini amefunga au kutengeneza goli, ukitizama benchi la Yanga na Simba, utagundua tatizo la simba ni usajiri tu!
Timu kama Azam FC ambayo misimu 6-7 nyuma ilikuwa haipat hata sare kwenye mechi za ligi kuu (2+1 fa) za msimu, leo wanaisumbuwa simba “home and away” kwa sababu ni usajiri tu!
Msimu huu azam wametufunga mara mbili na sare moja tena ya jasho na damu yote ni kwa sababu ya usajiri wao mzuri, usiniambie kuhusu kukamata nafasi ya pili, ukitaka kujuwa tazama wachezaji mmoja mmoja wa Azam, pale kwa Akamiko, Issah Ndala, Soss Bajana, pamoja na kipa wao Idrisu, utapata majibu ni kwanini nimekwambia “ilikuwa usajiri tu”.
Binafsi naamini viongozi washajuwa wapi kuna tatizo, nategemea watakuwa wamejifunza kwenye suala la usajiri, tunaposema usajiri ni ule unaoendana na hadhi ya klabu, tusiwe wabahili.
Yanga walitoa takribani Sh milioni 500 kwa mchezaji mmoja tu (Ki Aziz) na leo hii wanauhakika wa ubingwa wa ligi kuu kwa msimu wa pili mfululizo na rekodi wameweka kwenye michuano ya CAF, hii yote ni kwa sababu ya usajiri mzuri na kutokuwa na maneno mengi.