Mobile

Hakika Msimu Ujao wa Ligi Kuu Utakuwa wa Moto Sana....




Hivi unapata picha jinsi msimu ujao utakavyokuwa kutokana na uwepo wa baadhi ya makocha wakubwa? Umeshajiuliza hilo swali na kupata majibu yake, ujue itakuwa sio poa kabisa! Kama vipi msimu uanze tu 😆

MIGUEL GAMONDI yupo zake Singida Black Stars kwa wakulima wa alizeti na wafugaji wa kuku wa kienyeji 🙌🏾 bila shaka Gamondi atataka kuthibisha yeye ni kocha bora, ubora wake sio tu kwa sababu alikuwa Yanga.

FADLU DAVIDS kabakia Simba kila mtu ameona alichofanya kwenye msimu wake wa kwanza kwenye Ligi ya Tanzania na Kombe la Shirikisho Afrika. Akifanya maboresho kwenye mapungufu aliyoyaona msimu uliomalizika huenda akakimbiza tena.

FLORENT IBENGE ni kocha mshindani, hata kubali kuharibu wasifu wake mkubwa alioujenga kwa muda mrefu kwa hiyo atataka kuonesha ukubwa wake.

YANGA tayari kuna tetesi za makocha wenye wasifu mkubwa wanatajwa kuchukua nafasi ya Miloud Hamdi, atakaepata nafasi atataka kuendeleza kile kilichofanywa na watangulizi wake.

Naamini ligi kuu Tanzania Bara 2025|26 itakuwa tamu sana! Ushindani utakuwa mkubwa sana hususan kwa mafahari wanne [Yanga, Simba, Azam na Singida Back Stars] kwenye mbio za ubingwa.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad