Mobile

Fabrice Ngoma Mkali wa Bolu Aliyeacha Alama Simba

Fabrice Ngoma Mkali wa Bolu Aliyeacha Alama Simba


Unakumbuka lile vaibu la Yanga kutaka kutambulisha jezi namba 6 misimu miwili iliyopita? Yanga ilijinasibu na kutangaza ilikuwa mbioni kushusha namba 6. Lakini mambo yakaenda kinyume baada ya namba 6 iliyotarajikutua Jangwani ikaibukia Msimbazi.


Simba ilimtangaza namba sita huyo ambaye ni Fabrice Ngoma na watani zao waliishia kumtambulisha Skudu Makudubela aliyepewa namba 6, ingawa kiasili alikuwa kiungo mshambuliaji na winga tofauti na Mkongomani huyo aliyetokea Al Hilal ya Sudan.


Kama utani misimu miwili imeisha Ngoma akiwa Msimbazi na juzi kati amewaaga Wanasimba kuonyesha hatakuwepo katika kikosi hicho msimu ujao.


Kiungo huyo fundi mwenye miaka 31, Kupitia kipaji haiba yake nje ya uwanja na maneno mazito aliyoandika wakati wa kuaga, Ngoma ameacha kumbukumbu ya mchezaji aliyekuwa na weledi, utu na moyo wa shukrani.


Kuondoka kwa Ngoma siyo suala la kiufundi pekee, bali kiakili. Simba inahitaji siyo tu kujaza nafasi uwanjani, bali uongozi wa wachezaji. Mchezaji kama Ngoma hakujiamini yeye binafsi aliwajengea wengine kujiamini. Hii ni tabia adimu na ngumu kurithi.


Kocha Fadlu atahitaji kufikiria nani anaweza kuchukua nafasi yake, hasa kwenye mechi kubwa ambazo zinahitaji uzoefu, uelewa na uthabiti wa kimbinu. Simba inaweza kumsajili mchezaji mpya, lakini kiungo mwenye mchanganyiko wa ukomavu, nidhamu na utu kama wa Ngoma ni nadra kumpata


Safari ya Ngoma Simba imekamilika ikiwa haina mgogoro au kushuka kiwango, bali kwa staha, heshima na moyo wa shukrani. Katika kipindi kifupi amekuwa kioo cha nidhamu na mfano wa kuigwa. Ameondoka akiacha ujumbe ambao utadumu kwa muda mrefu: “Msiiache hii timu… nyakati nzuri zinakuja.” Haya si maneno tu, bali ni baraka kutoka kwa mtu aliyekuwa ndani ya mfumo anayeamini Simba bado ina safari ndefu ya mafanikio mbele yake

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad