Mobile

Aziz K Kuachwa na Wydad Kisa Kiwango Kidogo cha Bolu

 

Aziz K Kuachwa na Wydad Kisa Kiwango Kidogo cha Bolu


Klabu ya Wydad Athletic ya Morocco ipo kwenye mchakato wa kupunguza idadi ya wachezaji wa kigeni katika kikosi chake, ili kukidhi kanuni za Ligi kuu ya Morocco (Botola Pro) inayohitaji wacheza 5 tu wa Kigeni


Kufuatia kumalizika kwa michuano ya Kombe la Dunia la Klabu, Wydad ilikuwa na jumla ya wachezaji 8 wa kigeni waliocheza katika mashindano hayo:

Selemani Mwalimu, Guilherme Ferreira, Bart Meijers, Mickaël Malsa, Samuel Obeng, Stephane Aziz Ki, Pedrinho, na Arthur.


Tetesi zinasema Stephane Aziz Ki anatajwa kuwa kwenye orodha ya kuachwa baada ya kocha kutoonyesha kuridhishwa na kiwango chake.


Thembinkosi Lorch, ambaye ni mchezaji wa mkopo, anapangwa kupelekwa kwa mkopo sehemu nyingine.


Selemani Mwalimu, chipukizi kutoka Tanzania, anatarajiwa kupelekwa kwenye timu ya vijana ya klabu hiyo kwa ajili ya maendeleo zaidi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad