Simba Walikosa Kombe Ligi Kuu Msimu wa Nne Mfululizo….

 



Wananchi, Young Africans Sc wametwaa ubingwa wa Ligi Kuu bara kwa msimu wa nne mfululizo baada ya kuilaza Simba Sc bao 2-0 kwenye mchezo wa kufunga pazia la Ligi hiyo.


Simba Sc imetoka ‘kapa’ kwa msimu wa nne mfululizo kwenye Ligi Kuu huku Wananchi wakitwaa kombe hil kwa mara ya 31 kihistoria. Yanga Sc wamemaliza msimu kileleni wakiwa na pointi 82 huku Mnyama akimaliza nafasi ya pili pointi 78 baada ya mechi 30.


Jean Charles Ahoua amemaliza kama mfungaji bora wa Ligi hiyo akifikisha magoli 16 kwenye Ligi Kuu huku kipa wa Simba Sc Moussa Camara akimaliza kama kinara wa ‘clean sheets’ baada ya kucheza mechi 19 bila kuruhusu bao


FT: Yanga Sc 2-0 Simba Sc

⚽ 66’ Pacome (P)


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad