Mwenyekiti wa Bodi ya LIGI Mguto Ajiuzulu, Kasongo Asimamishwa Kazi

Mwenyekiti wa Bodi ya LIGI Mguto Ajiuzulu, Kasongo Asimamishwa Kazi


Kupitia taarifa kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imeelezwa kuwa Rais wa TFF Wallace Karia amemsimamisha kazi Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Almasi Kasongo.

Sambamba na hilo, Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi TPLB, Steven Mnguto naye amewasilisha barua rasmi ya kujiuzulu nafasi yake, huku TFF ikipokea uamuzi huo.

Taarifa hiyo imetolewa leo Juni 13, 2025 na Katibu Mkuu wa TFF, CPSP (T) Kidao Wilfred.

Wakati Huo huo BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeusogeza mbele mchezo namba 184 wa Ligi Kuu ya NBC kati ya klabu ya Yanga na klabu ya Simba ambao ulipangwa kufanyika kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Juni 15, 2025 kuanzia saa 11:00 jioni.

Mchezo huo sasa utafanyika Juni 25, 2025 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia saa 11:00 jioni.

Bodi inazitakia maandalizi mema klabu za Yanga na Simba kuelekea mchezo huo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad