Pamba Jiji wamestahili kufungwa mabao 5 na Mnyama,Walikua na makosa mengi mno ya kiulinzii..mfano halisi ni nyanda wao…Walikua na makosa mengi na hawakua na umakini katika kuzuia na mipango yao haikua thabiti mbele ya Mnyama waliyokuwa bora na imara katika dakika zote 90.
Simba SC na maana halisi ya Timu kubwa na yenye kikosi kipana..Licha ya kucheza mfululizo “Bila kupumzika” wamekua wakipata ushindi na kuendelea kusogea juu na kuwakaribia Yanga SC.
Leo Pamba Jiji walizidiwa maeneo yote,Wachezaji wa Simba SC walikua katika ubora mkubwa.
Ushindi huu wa Simba SC unawafanya wafikishe alama 66 na mabao 50 huku jumatatu wakimalizia kiporo chao dhidi ya KMC na endapo wakishinda watakua wameachwa na watani zao Yanga SC kwa alama 1.
Note:Jean Charles Ahoua kawekw kambani mara 3 na kufikisha mabao 15 akiwa ndiyo kinara wa ufungaji na ndiyo nyota wa mchezo wa leo.
Leonel Ateba akiweka kambani 2 na kufikisha mabao 12 katika Ligi akiwa nyuma ya Clement Mzize mwenye mabao 13 na kinara wao ni Ahoua.
Simba SC dakika za jioni walijisahau wakapigiwa shambulizi moja na wakafungwa bao 1 na Mousa Camarra kukosa cleen sheet…Huku Pamba Jiji wakipata on target moja tu na hiyo ndiyo ikawapa bao.
FT:Simba SC 5:1 Pamba Jiji.