Kundi la Ngorongoro Heroes ni la Kifo Aisee......



MICHEZO:Timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ‘Ngorongoro Heroes’ imepangwa kundi A katika fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana wa umri huo (AFCON U20) 2025 zitakazofanyika Misri baadaye mwezi huu.

Kundi hilo A linaundwa na timu tano ambazo ni Misri, Zambia, Ngorongoro Heroes, Sierra Leone na Afrika Kusini.

Ni kundi lenye mchanganyiko wa timu zenye uzoefu na mafanikio kwenye mashindano hayo na nyingine zinashiriki kwa mara ya kwanza.

Mwenyeji Misri ndio timu tishio zaidi katika kundi hilo kwa vile inashika nafasi ya pilk kwa kutwaa taji hilo mara nyingi ikifanya hivyo mara nne ambazo ni 1981, 1991, 2003 na 2013.

Misri imeshika nafasi ya pili mara moja na imewahi kumaliza katika nafasi ya tatu mara tatu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad