Ni usku wa kutisha, usku ambao waliowengi wamepumzika huku wakiwa hawana uhakika wa kuiona kesho yao ni usiku ambao Mungu pekee ndio anayejua nani na nani wataiona kesho, hakika usiku ni fumbo kubwa kwa binadamu.
Nikiwa kwenye dimbwi la usingizi naiskia sauti kwa mbali, sauti ambayo ilikuwa inaongea kwa shida sana lakini nilikuwa nasikia anachozungumza, ni sauti ya kikongwe aliyetokea kwenye kuta ya chumba changu kilionekana kivuli tu ila mwenyewe sikumuona, hakika nilistuka na usingizi ulikata.
Ile sauti ilikuwa inasema kijana amka nakutuma ukaseme ukweli kupitia mikono yako, nenda kazungumze ukweli ambao wengi hawataki kuusema na kama wanaujua wamechagua kukaa kimya, mjukuu wangu nenda kaseme ukweli huu.
Nenda kawaambie watanzania wampe thamani anayostahili huyu kijana kutoka Morogoro @jobdick05 nenda kawaambie ukweli kuwa huyu kijana sio beki tu lakini pia ni kiongozi wa mfano, nenda kawaambie kuwa huyu kijana msamiati kushuka kiwango haujawahi kutumika kwake, nenda kaseme.
Nisikilize nenda kawaambie watu kuwa huyu @jobdick05 tangu amejiunga na Yanga hakuna msimu amekaa nje kwa sababu ya kushuka ubora, waambie msimu wa nne na nusu sasa anawatumikia wananchi na anaanza kikosi cha kwanza kila kocha aliyepita jangwani amekiri ubora wa beki huyo.
Nenda kawaambie hao watanzania kupitia kalamu yako kuwa tuliwahi kuona mabeki bora sana enzi za nyuma akina Canavarro, Kelvin Yondani na wengine wengi ila kwasasa wakubali kuwa Dickson Job ndio beki bora kwenye ligi kuu.
Kama kuna mtu atakuuliza kuhusu huo ubora wake ni kwa wazawa au wakigeni? Mwambie hivi ni beki bora kwa wachezaji wote wanaocheza eneo lake haijalishi ni mzawa au mgeni.
Nenda kawaambie kuwa mizimu imechukia huku wanapoimbwa hao wengine na kusahau ubora na muendelezo anaoonyesha huyu kijana, kama mnataka awe mgeni ndio muimbe jina lake tuambieni tumchukue tumpeleke nje aje kwenye ligi kama mchezaji wa kigeni pengine mtaimba na kusifu jina lake.
Nenda mashariki, nenda Kaskazini Dickson Job ndio beki wa mfano kwa sasa kwenye ligi kuu, tunafurahi kama mizimu kuona kijana kutoka kwenye ardhi yetu anaitendea haki bendera ya Tanzania kwenye ngazi zote.