Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Alhamisi hii ya Oktoba 10, 2024 inatarajiwa kuwa na kibarua kigumu ugenini dhidi ya Timu ya Taifa ya DR Congo katika katika mchezo wa tatu wa kundi H kuwania tiketi za kushiriki michuano ya AFCON 2025 inayotarajiwa kufanyika nchini Morocco.
Taifa Stars inaingia katika mchezo huo ikiwa na historia mbaya dhidi ya wapinzani wao ya kutokushinda mchezo wowote wa kiushindani kwa zaidi ya miaka mitano sasa.
Katika michezo mitatu iliyopita kati ya Timu ya Taifa ya Tanzania na DR Congo, Timu ya Taifa ya DR Congo imefanikiwa kuibuka na ushindi mara moja na kutoka sare katika michezo miwili ikiwemo ule wa kundi F katika michuano ya AFCON 2023 iliyofanyika nchini Ivory Coast.
Katika mchezo wake uliopita, Taifa Stars ilifanikiwa uliopita kupata ushindi mgumu ugenini dhidi ya Timu ya Taifa ya Guinea katikika mchezo uliocheza Ivory Coast na kuwasogeza vinana hao wa Hemed Morocco hadi nafasi ya pili ya msimamo wa kundi H wakijikusanyia alama 4 kufuatia suluhu ya bila kufunana katika mchezo wa kwanza dhidi ya Ethiopia uliochezwa Septemba 4, 2024 katika Dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Wenyeji wa Taifa Stars, DR Congo ndio vinara wa kundi H wakiwa na alama 6 baada ya kushinda michezo yote miwili dhidi ya Guinea nyumbani na ugenini dhidi ya Ethiopia, mchezo uliochezwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar Es Salaam.