Simba Wameruhusu Goli Moja tu ‘FA’ kabla mechi na Azam FC

Simba Wameruhusu Goli Moja tu ‘FA’ kabla mechi na Azam FC

Kikosi cha Simba SC leo saa 9:30 Alasiri kitashuka katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona kuikabili Azam FC kwenye mchezo wa nusu fainali ya Azam Sports Federation Cup (ASFC).

Kabla ya mchezo wa leo wamecheza mechi nne ambazo zimewapa tiketi ya kukutana na Azam kwenye mechi ya nusu fainali.

Hatua ya 64…………

Simba 8-0 Eagle FC

Mchezo wa kwanza wa ASFC ulikuwa dhidi ya Eagle FC uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Disemba 10, 2022 ambao ulikuwa hatua ya 64 bora na tulishinda mabao 8-0.

Mabao yakifungwa na

Moses Phiri ⚽⚽⚽⚽

Clatous Chama ⚽⚽

Habib Kyombo ⚽

Pape Sakho ⚽

Hatua ya 32……………

Simba 1-0 Coastal Union

Mchezo wa hatua ya 32 bora dhidi ya Coastal Union ulipigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Januari 28, 2022 na walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao moja.

Sadio Kanoute ⚽

Hatua ya 16…………….

Simba 4-0 African Sports

Mchezo wa hatua ya 16 bora ulipigwa Machi 2, 2023 katika Uwanja wa Uhuru na kuondoka  na ushindi wa mabao 4-0.

Mabao yakifungwa na

Jean Baleke ⚽

Kennedy Juma ⚽

Mohamed Mussa ⚽

Jimmyson Mwanuke ⚽


Robo fainali………………….


Simba 5-1 Ihefu


Mchezo wa robo fainali uliopigwa katika Uwanja wa Azam Complex, Aprili 7, 2023 na tuliibuka na ushindi wa mabao 5-1.


Mabao yakifungwa na


Jean Baleke ⚽⚽⚽

Saido Ntibazonkiza ⚽

Pape Sakho ⚽


Mpaka wanaingia kwenye mchezo wa leo wa nusu fainali wamefunga mabao 18 na kuruhusu bao moja.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.