Simba Vs Azam Leo Mtanange wa Nguvu, MBrazil Apania Kuuwa Mtu Kwa Rungu, Beleke Saidoo na Chama Mguu Sawa

Simba vs Azam

Mitambo ya mabao ndani ya kikosi cha Simba SC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Roberto Oliveira imeandaliwa kuimaliza Azam FC leo Jumapili (Mei 07) wakati wawili hao watakapokutana kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’.

Ni Clatous Chama ambaye ni namba moja kwa kutengeneza pasi za mabao akiwa nazo 14 kibindoni na ametupia mabao matatu.

Jean Baleke mwenye mabao nane akiwa ametoka kufunga mbele ya Namungo FC na Shomari Kapombe mwenye pasi sita za mabao akiwa amesepa na dakika 1,867 naye anawavutia kasi Azam FC.

Meneja wa Idara ya Habari na Mwasiliano wa Simba Ahmed Ally amesema kuwa wanatambua mchezo wao dhidi ya Azam FC utakuwa mgumu lakini wapo tayari kwa ajili ya kupata matokeo mazuri.

“Mchezo dhidi ya Azam FC ni mgumu tunawaheshimu wapinzani wetu lakini tunahitaji ushindi ili tufike hatua ya Fainali kwani wachezaji wapo tayari na benchi la ufundi linaendelea na program zao.” amesema Ahmed Ally.

Timu hizo zinakutana huku Azam FC ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza bao 1-0 katika hatua ya Nusu Fainali ya michuano hii msimu wa 2020/21, lililofungwa na mchezaji wake wa zamani, Luis Miquissone baada ya mabeki kuzembea.

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Majimaji mjini Songea Mkoani Ruvuma, Miquissone alifunga bao hilo dakika ya 89 baada ya mchezaji wa zamani wa timu hiyo, Bernard Morrison anayeicheza Young Africans kwa sasa kuanzisha kwa haraka mpira wa kutenga ‘Free-Kick’.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad