Dodoma Jiji FC Yakataa Kuwa Ngazi ya Ubingwa Kwa Yanga


Published from Blogger Prime Android App


Uongozi wa Dodoma Jiji FC umeweka wazi kuwa wanahitaji alama tatu muhimu dhidi ya Young Africans ambao watacheza nao kesho Jumamosi (Mei 13), kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi  jijini Dar es salaam.

Dodoma Jiji ipo nafasi ya 10 baada ya kucheza mechi 27 ina alama 31 na Young Africans ambayo iko kileleni na alama zake 71 kama ikishinda mchezo huo basi atakuwa Bingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu 2022/23.

Afisa Habari wa Dodoma Jiji FC Moses Mpunga amesema kuwa, wanatambua juu ya mchezo wao dhidi ya Young Africans na wapo tayari kupata alama tatu muhimu.

“Mchezo wetu dhidi ya Young Africans ni muhimu kushinda kwa kuwa tunahitaji pointi tatu, tunatambua ni timu imara inafanya vizuri kwenye mashindano ya ndani nay ale ya kimatafa lakini tumejipanga.

“Ilikuwa hatujajua siku ya kucheza nao lakini kwa sasa ratiba ipo wazi hivyo inatufanya tuwe tayari kuikabili timu hiyo na wachezaji wapo tayari kwa mchezo wetu mgumu,” amesema Mpunga

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.