Seleman Mwalimu Gomez ni Balaa, Anahitaji tu Muda na Nafasi Ndani ya Simba, Tanzania Itamuimba

Seleman Mwalimu Gomez ni Balaa, Anahitaji tu Muda na Nafasi Ndani ya Simba, Tanzania Itamuimba


Natamani Tanzania ingekuwa kama Uingereza namna ambavyo wamekuwa na moyo mkunjufu wa kuwasapoti wachezaji wao wa kizawa na kuwapa promo kubwa kuliko hata uwezo wa mchezaji


Ukweli ukimuangalia namna ambavyo anacheza Seleman Mwalimu hakuna mshambuliaji ndani ya Simbasc ambaye anafikia ubora ambao yuko nao


👉 Uwezo wa kucheza kwenye eneo kubwa la uwanja

👉 Uwezo mkubwa wa kunusa hatari

👉 Ubora kwenye kumalizia nafasi

👉 Uwezo wa kubadilisha nusu nafasi na kuwa nafasi kamili

👉 Kucheza namba zaidi ya moja 7,10,11,9

👉 Uwezo mzuri wa kutumia miguu yote miwili

👉 Aina yote ya mipira anaweza kufunga (kichwa na miguu)

👉Kasi na nguvu

👉 Beki wawili mpaka watatu sio kitu kwake


Ukiangalia kwa aina ya washambuliaji ambao wako kwenye kikosi cha simbasc utagundua mwalimu ni bora zaidi ya wote


Changamoto ya Mwalimu ni Utanzania wake ambao yuko nao wenda angekuwa anatoka nje ya mipaka ya Tanzania angepewa nafasi kubwa kwenye kikosi


Ukweli mara chache sana kwa miaka ya hivi karibuni timu zetu za simba na yanga kuamini mshambuliaji mzawa wa kati


Maana hata Yangasc wana Mzize lakini achezi kama namba 9 mara nyingi utokee pembeni mara chache ndiyo upata nafasi hiyo ya kucheza kati kwa zalula


Naamini kama Simbasc wakampatia vitu viwili kwa maana ya nafasi ya kucheza na muda wa kumvumilia basi watavuna matunda kwa kijana huyu wa kitanzania.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad