Kocha Nasreddine Nabi Aikana Yanga Mchana Kweupe, 'Nimekuja Bongo Kwa Mambo Yangu Mengine'




Mara baada ya kocha mkuu wa Yangasc Romain Folz kuwa na kiwango ambacho sio cha kuridhisha kwenye michezo kadha ambayo ameisimamia klabu hiyo hatimaye uongozi wa Yangasc umeanza mchakato wa kutafuta mwalimu mpya ambaye atakuja kurithi mikoba ya mfaransa huyo


‎Na majina ambayo yanatajwa kwa ukubwa kikosini humo ni aliyekuwa kocha mkuu wa zamani wa klabu hiyo Nasreddine Nabi ambaye kwa sasa yupo nchini Tanzania

‎Lakini mara baada ya tetesi hizo Kasaco media ilimtafuta kocha huyo hili kuja ukweli wa taarifa

‎Nabi alisema “Nimeona watu wanasema nimekuja hapa kwa ajili ya Simba, wengine wanasema Yanga, hapana! Nipo hapa kwa safari yangu binafsi, nadhani hii ni mara ya tatu nakuja hapa,

‎“Tanzania ni nyumbani ndio maana napenda sana kuja hapa, tangu nimefika sijakutana na kiongozi yeyote wa Simba wala Yanga, nikimaliza mambo yangu nitaondoka.” ALISEMA NABI

‎Lakini pia  jina lengine ambalo lipo mezani kwa Yangasc ni la kocha mkuu wa kikosi cha Gaborone United ya nchini Botswana ambaye siku chache alikuwa nchini akikiongoza kikosi hicho kwenye ligi ya mabingwa barani Afrika mbele ya kikosi cha simbasc Dimitar Pantev raia wa Ubelgiji

‎Mpaka hivi sasa uongozi wa Yangasc aujatoa taarifa yeyote kuhusu hatima ya Romain Folz lakini taarifa za ndani zinaeleza kuwa uongozi wanataka kuutumia muda wa international black kupisha kalenda ya fifa mwalimu mpya kuandaa kikosi hicho .

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad