Huu Hapa Wasifu wa Kocha Mpya Simba



Klabu ya Simba SC imefikia makubaliano na kocha raia wa Bulgaria 🇧🇬, Dimitar Pantev kuinoa timu hiyo akichukua mikoba ya Fadlu Davids aliyetimkia Raja Casablanca.

Kocha huyo atawasili nchini kesho tar 4 October kwa ajili ya kuanza harakati za kuinoa timu hiyo akitokea Gaborone United ya Botswana 🇧🇼.

Pantev atawasili na msaidizi mmoja kwani makocha wengine waliopo Simba SC bado wapo klabuni ikiwemo Selemani Matola na kocha wa viungo.

Wasifu wa Kocha Dimitar Pantev

Jina kamili: Dimitar Nikolaev Pantev
Tarehe ya kuzaliwa: 26 Juni 1976
Taifa: Bulgaria 🇧🇬
Leseni ya ukocha: UEFA “A Licence”

Mafanikio Makubwa

🏆 Ubingwa wa Cameroon (Elite One) msimu wa 2023/24 na Victoria United.
🏆 Ubingwa wa Botswana Premier League msimu wa 2024/25 na Gaborone United.
🏆 Ameshinda Ligi ya Futsal ya Bulgaria mara tano mfululizo (2011–2016) akiwa kocha wa Grand Pro Varna.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad