Mobile

Wachezaji CHAMA na Jonas Mkude Hawajailipa Yanga ndani ya Uwanja, Wameilipa Yanga Nje ya Uwanja

Wachezaji CHAMA na Jonas Mkude Hawajailipa Yanga ndani ya Uwanja, Wameilipa Yanga Nje ya Uwanja


Kwa siku za karibuni Yanga imefanikiwa kuwashawishi wachezaji wanaomaliza mikataba yao Simba kuelekea Jangwani.


1. Jonas Mkude

2. Clatous Chama

* Mohamed Hussein [sio rasmi]


Kwa Mkude na Chama hawakufikia matarajio ya wengi kutokana na kile walichokionesha/kukifanya wakiwa na jezi ya Yanga ukilinganisha na walivyokuwa Simba. Hata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza imekuwa changamoto.



Je, ni sajili za kumdhoofisha mpinzani kutokana na siasa za hizi klabu mbili? Kwa sababu kwa sasa story itakuwa mchezaji wao tumemchukua.


Ukirudi nyuma kidogo, wakati Yanga inamtaka Mkude akiwa kwenye ubora wake hawakufanikiwa hata kwa Mohamed Hussein wakati Yanga ikiwa na uhitaji nae haikufanikiwa. Wakati Simba wanawataka kweli hao wachezaji hawakuondoka.


Mkude na Chama hawajailipa Yanga, ila Yanga ilifanikiwa nje ya uwanja kutengeneza picha kwamba ina misuli mikubwa kiuchumi kuliko Simba lakini ndani ya uwanja Yanga haijapata thamani ya wachezaji hao ukilinganisha na gharama ilizotumia.


Ndio maana leo Yanga hawaoni hatari kumpoteza Chama kwakuwa wanajua hawezi kurudi Simba 😀. Kwa hiyo walifanikiwa kuwavuruga Simba kwamba mchezaji wetu anaondokaje halafu anaenda Yanga?

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad