KUONDOKA KWA NAHODHA MOHAMED HUSSEIN HAKUNA ALIYEPOTEZA..✍️
JUNI 23, 2014, mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe (sasa marehemu), alitangaza kumsainisha nyota wa miaka 18 kutoka Kagera Sugar, Mohamed Hussein ‘Tshabalala.
Ni Miaka 11 ya utumishi uliotukuka ndani ya Jezi hii tukufu ya Simba Sports.
Mohammed Hussein aliingia Kama dalili ya Mwanzo Mpya baada ya Msimu 2013/2014 Simba Sports Kumaliza nafasi 4 nafasi mbaya kwa Kipindi cha miaka zaidi ya 10.
Huu ni Msimu ambao Azam Fc ndo walikuwa Mabingwa ,Yanga Africa nafasi 2 huku Mbeya City wakishika nafasi ya 3 na Simba Sports nafasi ya 4.
Pamoja na Mohamed Hussein Simba Sports Msimu huo wa 2014/2015 ilisajili wachezaji 13 akiwemo Ibarahim Ajibu na Emmanuel Okwi.
Msimu huu Nahodha Mohammed Hussein anapoaga na Kuondoka ,Simba Sports wamekosa Ubingwa wa Ligi Misimu 4 Mfululizo.
Simba sports wamefungwa Mechi 5 Mfululizo na watani zao wa jadi Yanga Africa
Baada ya Miaka 11 pamoja ni Lazima hapa Kuwe na tafakari kwa PandÄ™ zote.Nikweli tunahitajiana?
Simba Sports inahitaji Mwanzo Mpya,na tangu Msimu uliopita wameanza usafi wanajenga upya Kikosi chao
Nahodha Mohammed Hussein nae anahitaji changamoto Mpya. Miaka 11 Mataji 12 chini ya Makocha 16.
Robo Fainali 7 za CAF na Msimu huu Fainali ya CAF Confederation Cup .Anaweza Kuamka asubuhi Kibinadamu na Kujiuliza natakiwa Kufanya nini zaidi ya hapa?
Najua haikuwa rahisi Kuachana na ndo maana imefika leo hapa. Vikao vya Kujaribu Kusaini Mkataba Mpya vilikuwa vingi Lakini Mwisho haya ni Maamuzi mazuri kwa PandÄ™ zote
ONE MORE ROUND OF APLAUSE KWA NAHODHA ZIMBWE JR