Taarifa za uhakika kutoka katika chanzo cha kuaminika cha habari za michezo nchini Tanzania zinaeleza kwamba klabu ya Yanga Sc imefikia makubaliano ya kuachana ramsi na aliyekuwa kiungo mshambuliaji wao raia wa nchini Zambia Clatous Chota Chama.
Chanzo cha taarifa hii kimeeleza wazi kwamba mkataba wa Chama ndani ya klabu ya Yanga Sc umemalizika rasmi na viongozi wa klabu hiyo hawana mpango wa kumuongeza mkataba mpya kutokana na sababu za kimaslahi.
Inaelezwa kwamba Chama alihitahi kupewa ofa nono ya mkataba mpya ili aendelee kusalia katika klabu hiyo ambayo ameitumikia kwa msimu mmoja pekee lakini viongozi wa klabu ya Yanga Sc hawakuwa tayari kukubaliana na mahitaji ya Chama badala yake wamemruhusu akatafute changamoto mpya kwenye klabu nyingine.
Chama anaamini kwamba bado anaweza kuwa mchezaji muhimu ndani ya klabu ya Yanga Sc na ndio maana aliweka mezani ofa kubwa ili aweze kupewa kandarasi mpya ya kuendelea kuwatumikia wananchi kuelekea katika msimu ujao wa mashindano.
Viongozi wa klabu ya Yanga Sc wao wanaamini kwamba Chama ameshuka uwezo wake na sasa timu timu inatakiwa kupata namba 10 bora zaidi yake ili aweze kuibeba timu kwenye michuano ya ndani pamoja na ile ya kimataifa.
Taarifa hii kwa kiasi kikubwa inatoa tafsiri halisi kwamba sinema ya soka la Chama katika ardhi ya Tanzania inaeelekea ukingoni kwa maana kwamba nyota huyo kwa sasa atakuwa amepoteza ubora na mvuto na ndio maana Yanga Sc hawajataka kuendelea kufanya naye kazi kuelekea katika misimu ijayo ya mashindano.