Mohamed Doumbia Apewa Miwili Yanga

Mohamed Doumbia Apewa Miwili Yanga


MABOSI wa Yanga wameendelea kufanya usajili wa kimya kimya kwa kumpa mkataba wa miaka miwili kiungo mshambuliaji raia wa Ivory Coast 🇨🇮 aliyekuwa amefichwa katika kambi ya timu akijifua hata kabla ya Dabi ya Kariakoo


Yanga imemsainisha mkataba wa miaka miwili Mohamed Doumbia mwenye umri wa 26 akiwa mchezaji huru baada ya kutemwa na klabu ya Majestic ya Burkina Faso.


Usajili wa Doumbia fundi ambaye ana kasi na uwezo wa kucheza namba nane na 10, unakuja kuongeza nguvu eneo hilo ambalo limeondokewa na Stephane Aziz KI aliyesajiliwa Wydad Casablanca.


Siku moja kabla ya Dabi, arena ilinasa taarifa za kiungo mshambuliaji huyo kufichwa kambini Yanga akijifua na nyota wa kikosi hicho kutokana na kuwa nje ya uwanja tangu Machi mwaka huu alipotemwa na Majestic, lakini akiwa ameshapita klabu ya Slovan Liberec ya Czech.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad