Kocha Hamdi Avunja Ukimya, Aanika Ukweli Kuondoka Yanga

Kocha Hamdi Avunja Ukimya, Aanika Ukweli Kuondoka Yanga


 AKIZUNGUMZA na Mwanaspoti, Hamdi alisema hakutarajia kuitema Yanga, isipokuwa kitendo cha mabosi wa klabu hiyo kumkaushia kuanza naye mazungumzo wakati mkataba ukiwa umemalizika, ilimfanya asisite mara mbili mara ofa ya Wamisri ilipotua mezani kwake.


Kocha huyo aliyepewa mkataba wa mwaka mmoja na Ismailia, alisema kipaumbele chake kilikuwa ni kuendelea kubaki ndani ya Yanga lakini hakukuwa na ofa yoyote kwa mabosi hao wa Jangwani.


Alifichua mbali na ofa ya Ismaily, lakini alikuwa na nyingine ya US Monastri ya Tunisia na ES Setif ya Algeria na klabu nyingine za Afrika Kusini, lakini alikuwa akitamani kuendelea kubaki Yanga, ila kwa vile hakukuwa na mazungumzo yoyote na uongozi hadi alipoamua kuondoka nchini.


“Nimefurahi kuwa sehemu ya kikosi cha mafanikio mataji matatu ndani ya muda mchache nikiwa na timu yenye CV kubwa kama Yanga ni furaha kubwa kwangu naamini timu hiyo ina uongozi bora na kikosi imara itatwaa sana mataji ya ligi hiyo,” alisema Hamdi na kuongeza;

“Ulikuwa msimu bora kwangu ndani ya Yanga nimejifunza mambo mengi sana na nilikuwa na ushirikiano mzuri kuanzia viongozi wachezaji hadi mashabiki nawatakia mafanikio mema kwa msimu ujao naamini bado wataendeleza ushindani wana uongozi imara na timu bora.”


Hamdi alisema mafanikio aliyoyapata ndani ya Yanga yametokana na ubora wa timu na uongozi sahihi ambao umewekeza nguvu ndani na nje ya uwanja kuhakikisha timu hiyo inafikia mafanikio, huku akiishukuru Yanga kwa kumpa nafasi na kumuamini alichokifanya ni sehemu ya uaminifu aliopewa.


Ukiacha kuiongoza Yanga katika mechi 13 na kushinda 12 ikitoka sare moja, pia aliiongoza timu hiyo katika mechi tano za Kombe la Shirikisho kuanzia hatua ya 32 Bora hadi fainali akishinda zote akivuna mabao 17 na kufungwa moja tu.


Katika Kombe la Muungano, kocha huyo aliiongoza Yanga kucheza mechi tatu akishinda zote, akianza kwa kuifunga KVZ kwa mabao 2-0, kisha kuing’oa Zimamoto kwa penalti 3-1 baada ya sare ya 1-1 ya dakika 90 na katika fainali ikaichapa JKU kwa bao 1-0 na kutwaa ubingwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad