BAADA ya kulazimishwa suluhu juzi dhidi ya Mashujaa FC kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma, klabu ya Azam FC imesema wanachokutana nacho sasa ni mapito tu na muda si mrefu watarejea kwenye kiwango chao na kuanza kupata matokeo mazuri.
Akizungumza baada ya mchezo huo wa juzi, ofisa habari wa klabu hiyo, Hasheem Ibwe, alisema Mashujaa waliingia kwa nguvu kwenye mchezo huo hasa baada ya kumbukumbu ya kipigo cha mabao 3-0 ilichokipata kwenye uwanja huo msimu uliopita.
Azam haijapata ushindi kwenye michezo miwili ya Ligi Kuu, ambapo Alhamisi iliyopita ilishindiliwa mabao 2-0 dhidi ya Simba katika mchezo uliopigwa, Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
"Ni suala la muda tu timu yetu itarudi kwenye kiwango chake, unakumbuka kuwa msimu uliopita tuliwafunga hawa Mashujaa mabao 3-0 hapa hapa, leo walijua nini kingeweza kuwatokea, wakajipanga vizuri na kupata suluhu, na mmeona baada ya mechi walivyokuwa wakishangilia, kama wamepata ushindi, tunajipanga katika mechi ijayo," alisema