Okrah Aiponza Yanga, Wapewa Siku 45 na FIFA

 

Okrah Aiponza Yanga, Wapewa Siku 45 na FIFA

Shirikisho la soka duniani (FIFA) limeitaka klabu ya Yanga kuilipa kiasi cha USD 80,000 sawa na Tsh Milioni 216 klabu ya Bechem United ya nchini Ghana, pesa ya malipo iliyosalia katika uhamisho wa Winga Augustine Okrah kutoka Bechem United kwenda Yanga.


FIFA imeitaka klabu ya Yanga kulipa pesa hiyo ndani ya siku 45 kuanzia sasa na tofauti na hapo Klabu ya Yanga itakumbana na adhabu kutoka FIFA.


Yanga ilimsajili Okrah Januari 2024 na kuachana nae mwishoni mwa msimu uliopita akifanikiwa kubeba Ubingwa wa Ligi Kuu NBC na Kombe la CRDB.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.