MVP Simba Awatoa Hofu Mashabiki

 

MVP Simba Awatoa Hofu Mashabiki

Baada ya Simba kuanza Ligi Kuu Bara kwa ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Tabora United, kiungo wa mpya wa kikosi hicho, Ahoua Charles amewatoa hofu mashabiki wao akisema hana presha na kiwango chake wala kikosi na ni suala la muda tu mambo yatakuwa matamu zaidi.


Katika msimu wa 2023/24 Ahoua aliibuka mchezaji bora (MVP) wa Ligi Kuu Ivory Coast akiichezea Stella Club, huku akifunga mabao 12 na kutoa asisti tisa.


Akizungumza na Mwanaspoti, mchezaji huyo ameeleza kuwa hana presha na kiwango chake, lakini anapambana kuzoeana na kujuana na wachezaji wenzake ambapo kumekuwa na mabadiliko makubwa kwenye kikosi chao kutokana na nyota wengi kuwa wageni akiwamo yeye.


Ameeleza kuwa kwa sasa anataka kuendelea kushika kwanza falsafa ya kocha, Davids Fadlu, lakini pia ameshaona ladha ya mechi za Ligi Kuu na ushindani ulivyo.


"Ndani ya muda mfupi ujao mashabiki wetu wataanza kuona mambo mazuri zaidi ya wachezaji wenzangu kwa sababu kazi ya kwanza ilikuwa ni kuanza vyema mashindano," amesema.


"Tuna kikosi imara sana chenye wachezaji bora ambacho kinaweza kusimamia malengo ya kwenda kuchukua mataji kwa msimu huu na kufika hatua nzuri katika michuano ya kimataifa."


Katika mechi dhidi ya Tabora United pasi nyingi ambazo zilikuwa zikipigwa katika eneo la kiungo, Steven Mukwala, Jean Charles Ahoua na Joshua Mutala walishindwa kuwa na uamuzi sahihi wa kuziunganisha kiasi cha mabeki wa Tabora kuwadhibiti.


Licha ya hayo mpaka sasa ana rekodi ya kuwa na asisti moja iliyosabishwa na mpira wa kona uliozaa bao la kwanza la Simba jana lililofungwa kwa kichwa na beki wa kati, Che Malone katika dakika ya 14.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.