Hivi Hapa Viingilia Yanga na Vitalo Kwa Mkapa

 

Hivi Hapa Viingilia Yanga na Vitalo Kwa Mkapa

Kuelekea mchezo wa marudiano kati ya Young Africans dhidi ya Vital’O Jumamosi ijayo, viingilio vimetajwa katika madaraja manne.


Kiingilio cha juu ni Tsh 30,000 katika Jukwaa la VIP A, huku kile cha chini kabisa Jukwaa la Mzunguko ikiwa ni Sh 5,000.


Mbali na hivyo, katika mchezo huo ambao tutakuwa wenyeji, Jukwaa la VIP B ni Tsh 20,000 na VIP C Tsh 10,000.


Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam kuanzia saa 1:00 usiku.


Ikumbukwe kwamba, katika mchezo wa kwanza uliochezwa Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam tukiwa wageni wa Vital’O, tulishinda magoli 4-0 yaliyofungwa na Prince Dube, Clatous Chama, Clement Mzize na Stephane Aziz K

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.