Azam FC: Hatujapokea PESA za Prince Dube

 

Azam FC: Hatujapokea PESA za Prince Dube

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Azam, Thabiti Zakaria Zaka Zakazi amesema kuwa bado hawajapokea malipo ya kuvunja mkataba kutoka kwa mchezaji Prince Dube.


Hivi karibuni ziliibuka tetesi kuwa tayari Mzimbabwe huyo ameshawalipa Azam kiasi ambacho wanakitaka ili wamwachie awe huru.


"Sisi bado tunamdai Dube pesa ambazo zimeandikwa kwenye mkataba, mkataba unasema atakaevunja mkataba anatakiwa kulipa dola za Marekani 300,000.


"Dube ameondoka wakati msimu unaendelea hivyo tunataka fidia, mpaka sasa sijapata taarifa zozote, muda ukifika tutatoa taarifa rasmi," Thabit Chumwi (Zaka Zakazi) afisa habari wa Azam FC.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.