Hatimaye Simba yafunguka ishu ya Kocha Mkuu

 

Hatimaye Simba yafunguka ishu ya Kocha Mkuu
Kocha Juma Mgunda

Hatimaye Simba yafunguka ishu ya Kocha Mkuu

Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmedy Ally kuhusu nafasi ya Kocha Mkuu wa timu hiyo amesema;


“Nafasi ya kocha mchakato wake utakamilika muda sio mrefu na tutamtangaza. Tutatangaza nafasi zote katika eneo la benchi la ufundi na sio Kocha Mkuu pekee.


“Najua maswali yamekuwa mengi kuhusu Kocha Juma Mgunda na Selemani Matola ambao kimsingi mpaka sasa ndio makocha wetu hadi pale itakapotangazwa vinginevyo.


“Mgunda amethibitisha ni kocha wa daraja la juu na shauku ya wanasimba wengi ni kuona anakabidhiwa timu moja kwa Moja.


“Swali hili la Mgunda na yale mengine yote kuhusu kocha tutayajibu siku sio nyingi,” amesema Ahmed Ally.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.