Tupo tayari Dube ama timu yake MPYA Watulipe kidogo kidogo - Azam FC

 

Tupo tayari Dube ama timu yake MPYA Watulipe kidogo kidogo - Azam FC
Prince Dube

 Tupo tayari Dube ama timu yake MPYA Watulipe kidogo kidogo - Azam FC

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Azam, Thabiti Zakaria Zaka Zakazi amesema kuwa bado hawajapokea malipo ya kuvunja mkataba kutoka kwa mchezaji Prince Dube.


Hivi karibuni ziliibuka tetesi kuwa tayari Mzimbabwe huyo ameshawalipa Azam kiasi ambacho wanakitaka ili wamwachie awe huru.


“Sisi hatuna matatizo na Dube, kijana wetu ambaye tumeishi naye vizuri sana lakini kilichotokea ni masuala ya kimpira. Yeye alifungua kesi TFF akitushtaki sisi kwamba ule mkataba tuliosaini yeye hakusaini, kwa hiyo mpaka sasa tunasubiri hukumu ya TFF yatoke na hakuna habari mpya.


“Hukumu ikitoka tutajua tunafanyaje, labda kwenda kupambania haki yetu mbele ama kuachana naye tu au alipe kidogo kidogo.


“Sisi tunatamani wachezaji nao wachezaji, ila tutafute namna yoyote ya yeye kutulipa kama hana pesa ya kutulipa sasa hivi hata klabu anayokwenda watatulipa kidogo kidogo sisi hatuna shida.


“Cha msingi tunataka mchezaji acheze na sisi tunacheza ndiyo maana tumefuzu champions League bila yeye,” amesema Zaka za Kazi," Thabit Chumwi (Zaka Zakazi) afisa habari wa Azam FC.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.